Mzuka wa FFU kuamia kwa washabiki!

Wasanii wa wa FFU wakiwa kazini jukwaani!

NGOMA Africa Band aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani,
Bendi hiyo maarufu barani ulaya itatingisha tena jukwaa la onesho
ya kimataifa la International African festival, mjini Tubingen, Ujerumani.

Onesho hilo litafanyika Agosti 11 na 12, 2012 katika uwanja wa
FestPlatz, Tubingen. Habari za uhakika zinaeleza kuwa bendi hiyo imechaguliwa kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya na kushinda tuzo la Award ya “IDA – International Diaspora Award”.
Tuzo hilo litakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki mahiri Kamanda Ras Makunja usiku wa Jumapili 2012, Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kimepigiwa kura nyingi na washabiki, pamoja na tahasisi mbalimbali kwa kutajwa kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya iliyoweza kutumia muziki wake kama daraja na kufanikiwa kuziteka nyoyo za washabiki na kuwaunganisha
washabiki wa mataifa mbali mbali duniani.

Pia kikosi kazi hiko kimetajwa mara nyingi kuwa kimediliki kujitoa muanga kwa kupiga muziki mpaka kwenye nchi zenye usalama mdogo na mazingira ya kivita! Kwa ujasili huu Ngoma Africa band inavuna inachopanda.

Ngoma Africa band imetajwa kuwa muziki wake umefanikiwa kuzoa mamilioni ya washabiki na kuchangia kwa kiasi kikubwa kutukomeza fikira za kiubaguzi wa rangi zilizomo kwa baadhi ya wazungu barani ulaya.

Ngoma Africa band inasemekana kuwa na washabiki au wafuasi milioni 50 dunia nzima,na washabiki wengine milioni 11 wanapitia tovuti ya bendi hiyo at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com

Miongoni mwa wapenzi hao ni wapo wanawake na wanaume, watoto, vijana na wazee wenye rika na mataifa mbalimbali, bila kujali itikadi za dini na matabaka ya maisha yao, wote wapo chini ya kivuli cha mzuka wa muziki wa Ngoma Africa Band a.k.a FFU inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja.

Usikose kuwasikiliza FFU katika www.ngoma-africa.com