Walimu waanza mgomo wao rasmi, wanafunzi waandamana

Wanafunzi shule za msingi

Waandishi Wetu, Moshi, Tanga, Iringa, Ruvuma na Dar

LICHA ya Serikali kukimbilia mahakamani na kusisitiza walimu wasigome, agizo hilo limepuuzwa kwa baadhi ya mikoa na hatimaye walimu kuanza mgomo uliozua maandamano ya wanafunzi. Baadhi ya walimu kutoka mikoa kadhaa waligoma kwa staili mbalimbali jambo ambalo kwa Ruvuma limesababisha maandamano kwa wanafunzi wakidai wanataka haki yao ya kufundishwa.

Kwa mujibu wa taarifa za waandishi wetu kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam, Iringa pamoja na Iringa wameshuhudia walimu wakiendesha mgomo wa staili anuai uliowaathiri pia wanafunzi.

Baadhi ya maeneo walimu walifika shuleni lakini hawakujishughulisha na kufundisha huku wengine kugoma kabisa kufika shuleni, jambo lililowafanya wanafunzi baadhi ya shule kuonekana wamelala na wengine kucheza michezo mbalimbali.

Kwa mkoani Kilimanjaro Wanachama hao wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wameunga mkono mgomo huo kwa zaidi ya asilimia 80, hali ambayo imeonekana kuwaathiri zaidi wanafunzi baada ya walimu wengi kufika shuleni na kukaa ofisini huku wengine wakigoma kufika kabisa.

Mgomo huo umesababisha Katibu wa CWT Wilaya ya Hai, Dauson Tem na Mwenyekiti wake, Terewandumi Swai kushikiliwa kwa mahojiano kwa kile kudaiwa kushinikiza mgomo kwa wenzake. Hata hivyo mtandao huu ulipomtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alikanusha kushikiliwa kwa viongozi kwa madai kuwa mgomo huo hauwahusu wao (polisi) hivyo hawawezi kuingilia.

Katibu wa CWT mkoani Kilimanjaro, Nathanael Mwandette alisema walimu waliopiga kura ni walimu 8,523 na kati ya hao walimu waliounga mkono mgomo ni 8,098 na kwamba mgomo huo ni halali kwa mujibu wa sheria.

Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Moshi inaongoza kwa zaidi ya asilimia 80 ikifuatiwa na Wilaya ya Same kwa asilimia 70, Hai asilimia 70, Mwanga asilimia 60, Rombo asilimia 50 huku katika wilaya ya Siha yenye shule za sekondari 14, shule 10 zikiwa zimefanya mgomo na shule nne kupinga mgomo huo.

Mwandette alikiri kuwepo kwa athari kubwa ambazo zinatokana na mgomo
huo na kusema kuwa pamoja na athari hizo bado hawataweza kuendelea na
kazi hadi pale ambap[o serikali itasikiliza kilio chao cha kuwaongezea
mshahara.

Aidha aliwataka walimu katika mkoa wa Kilimanjaro kupuuza vitisho
ambavyo vinatolewa na baadhi ya viongozi wa serikali kwamba mgomo huo
ni batili kutokana na kwamba wamezingatia taratibu zote ambazo
zinahitajika hivyo hakuna sababu ya kuogopa.

“Mgomo huu ni halali na si batili kama baadhi ya viuongozi wa serikali
wanavyosema, tumefuata taratibu zote ambazo tulipaswa kuzifaata
kisheria, na mgomo wa kipindi hiki tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kwani kuna baadhi ya shule ambazo walimu hawajafika kabisa shule na
kuna ambazo pia walimu wakuu hawajafika na tutaendelea hadi pale
ambapo serikali itatusikiliza na kutupa hakizetu,” alisema Mwandette.

Mwandishi ametembelea baadhi ya shule Kilimanjaro na kushuhudia wanafunzi wakiwa madarasani pasipo kufundishwa huku wengine wakionekana kuzurura maeneo ya shule.

Mkuu wa shule ya Sekondari Annamkapa iliyoko Kata ya Pasua Manispaa ya Moshi, Sindato Seiya alikiri kuwepo kwa mgomo na kuongeza kuwa kati ya walimu 38 ni walimu 26 tu walifika shule lakini hakuna aliyeingia darasani.
Hali hiyo ilikuwa vivyo hivyo shule ya sekondari Kiusa