Multichoice Tanzania ilivyofuturisha kukaribisha Olympics

Multichoice Tanzania ilivyofuturisha kukaribisha Olympics

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya futari wakati wa kukaribisha michuano ya Olympics iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar.

Barbara Kambogi ametumia fursa hiyo pia kuwataarifu Watanzania kuwa Kampuni yao pendwa ya Multichoice kupitia king’amuzi chao cha DStv inawaletea chaneli maalum itakayokuwa ikuzungumzia maadili ya Uislam katika kipindi hichi cha mfungo wa Ramadan ambacho pamoja na kuwakumbusha wakubwa pia tutawaelimisha watoto kujua nini wanapaswa kufanya ndani ya Uislam.

Alisema gharama za kufunga king’amuzi zimeshushwa na kufikia shilingi 169,000 ambapo atakayejiunganisha atafurahia chaneli nane za Super Sport zitakazokuwa zikonyesha michezo ya Omlympics iliyoanza jijini London kwa muda wa saa 24.

Pia amewakumbusha Watanzania wasisahau kua Kagame Cup iko live kupitia chaneli ya Super Sport 9 ya DStv.

Baadhi ya Waandishi habari kutoka vyombo mbalimbali nchini waliohudhuria hafla hiyo wakijisevia Futari.

Mkurugenzi wa Jambo Concept Benny Kisaka.

Huku wengine wakiendelea kubadilishana mawazo.

Waandishi wa habari wakienjoy futari iliyoandaliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania.

Katikati ni Issa Michuzi sambamba na Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto (kulia).