*Kutambulisha ‘Full Stop’ na Mjini Chuo Kikuu’
Na Mwandishi wetu
KUNDI la taarab la Tanzania One Thetre (TOT) chini ya Malikia wa Mipsho nchini, Khadija Omari Kopa litarindima katika mikoa ya Tanga na Kanda ya Ziwa baada ya mfugo huu mtukufu wa Mwezi wa Ramadhani.
Katibu wa TOT, Gasper Tumaini alisema, kwamba, ziara hiyo ambayo itatumika kutambulisha ambam za ‘Full Stop’ na ‘Mjini Chuo Kikuu’, itaanza kwa kundi hilo kurindima katika mkoa wa Tanga katika kurehekea Sikukuu ya Eid El Fitr.
Alisema, baada ya kuwakonga nyoyo wakazi wa Tanga na vitongoji vyake, Khadija Kopa na kundi lake watainua nanga na kwenda kuishusha tena Kanda ya Ziwa, katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara na kisha kumalizia Tabora na Singida.
Tumaini alisema, Idi pili TOTO watafunga kazi katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na kumalizia siku ya Iddi tatu katika ukumbi wa White House mjini Muheza mkoani Tanga. Alisema, mbali na Khadija Kopa, kundi hilo litakuwa nalo beneti, wanamuziki wake wa taarab, wakiwemo Abdul Misambano, Ally Star, Mwamtama Amir aka Mama Lao, Mariam Khamis na Mwasiti Suleimani.