Watanzania walivyowakumbuka mashujaa

Mnara wa Mashujaa uliopo katika viwanja vya Mnazi mmoja
Jijini Dar es Salaam,polipofanyika Maadhimisho ya siku ya Mashujuaa
leo,maadhimisho hato yalihudhuriwa na Mabalozi wa Nchi mbali
mbali,wananchi wa wawakilishi wa Dini mbali mbali na kuombewa dua hao
Mashujaa waliopoteza Roho zao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho
Kikwete akiweka Ngao na Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa,wakati wa
kumbukumbu ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika leo katika viwanja vya
Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam

Kiongozi wa Mabalozi Juma Khalfan Mpango,akiweka Shada la
Mauwa wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya
Mashujaa,yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi mmoja ulipojengwa
Mnara wa Mashujaa jijini Dar es Salaam

Makamo wa Rais wa Muungano Dk .Mohamed Gharib
Bilal,(kutoka kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi,Rais Msataafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi
na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho,wakiwa
katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika yaliyofanyika leo
katika Mnara wa Mashujaa Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.[Picha na
Ramadhan Othman,ORZ.]