KIKOSI cha timu ya taifa ya mpira wa miguu Tanzania kimefika salama Bangui, tayari kwa mchezo wake na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ikiwa ni mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) mwakani.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoituma jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bonifasi Wambura ambaye ameambatana na timu hiyo amesema wamefika salama na tayari wameanza mazoezi kujiandaa na mchezo wao unaofanyika leo.
Wambura amesema Kikosi cha Taifa Stars kimefikia Hoteli ya Hoteli ya De Centre kilifanya mazoezi katika uwanja ambao ndio utakaotumika kwa mpambano huo. Amesema mchezo huo unachezwa kesho majira ya saa 9 arasili saa za Bangui ikiwa ni sawa na saa 11 kamili, kwa saa za Tanzania.
Akizungumzia mchezo huo Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Poulsen amesema wamekwenda kwa lengo la kushinda, na atatumia mfumo ule ule wa uchezaji ambao tayari wachezaji wake wameuzoea, ili kufanya vizuri dhidi ya mahasimu wao.
Mchezo huu ni wa marudiano ambapo mchezo wa kwanza ulifanyika nchini Tanzania, Machi 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza.