Mwanafunzi IFM afariki kifo cha utata

Mwili wa Marehemu Agnes ukiwa kanisani tayari kwa heshima ya mwisho katika kanisa la Romani katoliki Mbezi Temboni.

Padre wa Parokia ya Mbezi Temboni akibariki mwili wa Agnes King’unza

Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.

Mama Mzazi wa Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa Mwanae


Marehemu Agnes B. King’unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mwili wa Marehemu Agnes King’unza umesafirishwa kwenda Nyumbani kwao Kalenga – Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika 19/07/2012.

Mwili wa marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.