TAARIFA ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba meli ya abiria iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar imezama na abiria zaidi ya 200. Meli hiyo iliyotambulika kwa jina la Mv. Karama inayomilikiwa na kapuni ya Seagal inadaiwa imezama ghafla baada ya kupinduka kichwa juu chini.
Taarifa za awali zinasema watu kadhaa tayari wamepoteza maisha baada ya ajali hiyo, vyombo vya uokoaji vimeshafika eneo la tukio kutoa msaada kwa waathirika wa ajali hiyo. Taarifa zaidi zinasema maiti kadhaa zimeanza kupokelewa bandarini Unguja.
Mtandao huu unaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa hizo na utakuwa ukiwajuza zaidi kuhusiana na tukio hilo kadri zitakavyo tufikia.