Camera ya dev.kisakuzi.com leo imeangalia Maonesho ya 36 Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Dar es Salaam
Mchambuzi wa Hesabu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Mariam Mtunguja (kulia) akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Fedha leo jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere.
Mtaalamu wa Uchumi, Idara ya Bajeti, Adamu Msumule (kushoto) akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Fedha leo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 36 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mauzo na Masoko David Manyanga (kulia) juu ya faida ambazo mkulima anaweza kuzipata baada ya kununua mashine ya kupanda mpunga aina ya SPW 48C wakati kiongozi huyo alipotembelea maonesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es Salaam leo katika Viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Fao la Matibabu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Aisha Marine (kushoto) jinsi wanachama wa mfuko huo wanavyonufaika na huduma hiyo wakati kiongozi huyo alipotembelea maonesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es Salaam leo katika Viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere. Katikati ni Ofisa wa NSSF anahusika na mambo ya Itifiki Juma Kintu. Picha zote na Tiganya Vincent – MAELEZO- Dar es Salaam