KAMPUNI ya Oriflame inayojishughulisha na kutengeneza vipodozi yenye makao yake makuu nchini Sweden, imezindua bidhaa mpya zitakazouzwa nchini kwa kupitia wasambazaji na wanachama wake.
Bidhaa hizo za Oriflame zinatengenezwa kwa kutumia matunda, maua na mimea mbali mbali inayoweza kusaidia ngozi kuwa katika hali bora na vilevile kukinga na kutibu maradhi mbalimbali ya ngozi.
Katika hafla hiyo watanzania wameshauriwa kutumia bidhaa za ngozi zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi halisi ili kuboresha na kuimarisha muonekano wa ngozi zao na kuepuka madhara yatokanayo na kemikali.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo ya uzinduzi, Shyrose Bhanji ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, amewasihi watu kupenda na kuthamini ngozi zao kwa kutumia bidhaa zisizokuwa na kemikali zenye kuleta madhara.
Aidha pia amewashauri watanzania wajiunge na biashara hii ya mtandao ambayo itawaingizia kipato kwa wingi na vile vile wataweza kutunza urembo wao wa asili kwa kutumia bidhaa wanazoziuza ambazo wao hupata kwa bei ya punguzo tofauti na wateja wasio wanachama.
Bidhaa ambazo zimezinduliwa kwa mara ya kwanza ni pamoja na Manukato(Pafyumu), mafuta ya ngozi maalum kwa uso, vipodozi vya usoni kwa wanawake na wanaume na pia mafuta maalum ya kupaka wanaume baada ya kunyoa ndevu. Uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es salaam umehusisha Wanachama, wasambazaji na wageni mbalimbali.
Kuhusu Oriflame:
Oriflame (EA) Tanzania Limited ni tawi la Oriflame East Africa ambayo makao yake makuu yapo nchini Sweden. Oriflame Tanzania imefunguliwa mwaka 2011 mwezi May, ambapo mpaka sasa imeweza kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfu saba (7000) ikiwa ni kama wanachama, wasambazaji, na waajiriwa wa kudumu.
Malengo ya Oriflame ni kuwa kampuni namba moja duniani inayofanya biashara ya vipodozi kwa namna ya mtandao (Network Marketing)