Tamasha la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza mkoani Mbeya

Wachezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Manchester City ya Uingereza wakichuana vikali na mchezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Real Madrid huku wakati wa tamasha la mashabiki wa vilabu vya Ulaya linalojulikana kama Serengeti Fiesta Soccer Bonanza, ambalo linafanyika jijini Mbeya katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu (TIA) na kushirikisha timu za mashabiki wa vilabu vya Manchester United, Liver Pool, Bayern Munichen, Asernal, Manchester City Barcelona, Chealsea na Real Madrid, Mshindi katika bonaza hilo atajishindia shilingi 500,000.
Wachezaji wa timu ya mashabiki wa Barcelona wakichuana vikali na wachezaji wa timu ya mashabiki wa Chealsea katika bonanza hili timu hizo ndiyo zilizofungua dimba.
Mratibu wa Serengeti Fiesta Soccer Bonanza Shafii Dauda akitoa maelekeza kwa timu za mashabiki wa Chealsea na Barcelona kabla ya kuanza kwa mtanange wao.
Timu ya mashabiki wa Manchester Unitedi wakishangilia wakati wimbo wao ulipokuwa ukipigwa.