Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi akiwa na naibu wake Mhe Pereira Silima (wa kwanza kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Fakihi Jundu (wa pili kulia) wakiwa meza kuu na Kamishna Jenerali wa Magereza anayemaliza muda wake, Afande Augustine Nanyaro (wa tatu kulia) katika hafla ya kumuaga kiongozi huyo wa magereza anayestaafu rasmi mwishoni mwa mwezi huu baada ya kutumikia jeshi hilo kwa takriban miaka 37. Hafla hii ilifanyanyika usiku wa kuamkia leo katika Bwalo la Maafisa wa Magereza la Ukonga, Dar es salaam