TIMU ya Taifa la Hispania hatimaye imekata mzizi wa fitina baada ya kunyakuwa la UEFA-EURO baada ya kuichakaza bila huruma timu ya Taifa la Italia.
Hispania wamefanikiwa kutwaa kombe hilo tena wakiwa mabingwa watetezi baada ya kuifunga Italia mabao 4-0, mchezo ambao ulionekana kuwa mwepesi kiushindi kwa Hispania tangu dakika 14 ya mchezo.
Hispania walioonekana wakicheza kwa kwa kujiamini walianza kuandika goli la kwanza dakika 14 ya mchezo, lililofungwa na David Silva huku la pili likifungwa na Jordi Alba. Hadi kipindi cha kwa kinamalizika Hispania ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili. Kipindi cha pili kilionekana kuwa kihama kwa Timu ya Italia, kwani ilijikuta ikiongezwa mabao mawili tena huku wafungaji wakiwa ni Fernando Torres, Juan Mata.
Hispania waliwakilishwa na Casillas 7, Arbeloa 7, Pique 7, Ramos 7, Alba 8, Busquets 8, Alonso 8, Xavi 9, Silva 8 (Pedro 5), Iniesta 8 (Mata 7), Fabregas 8 (Torres 8) na Pique.
Italia waliwakilishwa na Buffon 5, Abate 6, Barzagli 5, Bonucci 5, Chiellini 4 (Balzaretti 5), Pirlo 5, Marchisio 5, Montolivo 5 (Motta 3), De Rossi 6, Balotelli 4, Cassano 5 (Di Natale 6), pamoja na Barzagli.