Lisa Jensen mgeni rasmi Redd’s Miss Mara 2012

Na Mwandishi wetu
Musoma,

Mnyange anayekwenda kuiwakilisha Nchi katika mashindao ya miss world 2012 Nchini China mapema mwezi wa nane na miss Mara mwaka 2006 ambaye ni mshindi wa tatu katika miss Tanzania mwaka 2006 Lisa Jensen amewasili Mkoani Mara kwa ajili ya kushuhudia kinyang’ang’anyiro cha kumpata miss Mara 2012 akiwa kama mgeni rasmi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika uwanja wa ndege Musoma Lisa alisema anawashukuru waandaji wa miss Mara kampuni ya Homeland kwa kumpa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika shindano hilo na kueleza kuwa hiyo ni heshima kubwa kwake na ameshukuru kupata heshima hiyo.

Alisema hiyo imeoonyesha mashindano ya urembo sio uhuni kama ambavyo bado kuna watu wenye mawazo kuwa urmbo ni uhuni na kudai kuwa hurka ya uhuni na ya mtu mwenyewe na unaweza kufanya mambo mengi ya kujiletea maendeleo kutokana na fani ya urembo.

Alidai kuwa kwa upande wake tangu aingie kwenye masuala ya urembo mwaka 2006 amepata faida kubwa kutokana na kuingia katika mikataba mbalimbali ya makampuni ya ndani na nje ya nchi na kujiingizia kipato na hii leo akiwa mrembo anayetokea mkoa wa Mara anakwenda kuiwakilisha Nchi katika mashindano ya miss world huko nchini China mapema mwezi wa nane.

Lisa aliwataka warembo wanaoshiriki shindano la miss Mara mwaka huu kujiamini na kuyapa nidhamu mashindano hayo na kufanya kile ambacho kimewaingiza katika mambo ya urembo na watafika mbali kwani masula ya urembo tayari yametoa ajira mbalimbali kwa walio tangulia.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Homeland Godsos Mukama alisema maandalizi yote kuhusiana na shindano hilo yameshakamilika na kinachosubiliwa ni kufika siku ya ijumaa june 29 ili aweze kupatikana mrembo atakayeuwakilisha mkoa katika mashindano ya kanda na baadae miss tanzania.

Alisema kutokana na sifa walizonazo warembo wote 10 waliopo kambini anaamini mshindi atakayetwaa taji la miss Mara atakwenda kufanya vizuri katika mashindano ya kanda na baadae Taifa kama ambavyo alifanya Lisa Jensen.

Mukama aliongeza kuwa katika kusindikiza shindano hilo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wanaofanya vizuri katika muziki wa bongo freva hapa Nchini akiwemo Profesa J na Sharo millionea pamoja na dansa kutoka bendi ya twanga pepeta BOKI Bokilo.

Shindano la kumtafuta Reed’s Miss Mara 2012 litafanyika katika ukumbi wa Musoma club siku ya ijumaa ya june 29 kwa kiingilio cha shilingi elfu kumi.