Redd’s Miss Ubungo 2012 yapata wadhamini

Redd’s miss ubungo

JUMLA ya makampuni sita yaliyojitokeza katika udhamini wa Redd’s miss Ubungo msimu huu, makampuni hayo ni REDD’S, MBEKENYELA TRANSPORT, LADY PEPETA, FLEXIP, NAEEMS CLASSIC WEAR na CLOUD’S FM ndiyo yatakayo isukuma siku hiyo landmark hotel.

Warembo wapatao kumi na sita wamejitokeza kuwania taji hilo la redd’s miss Ubungo 2012 wakiwa chini ya mwalimu wao BEATRICE JOSEPH ambaye alikuwa Miss Ruvuma 2004.

Mashindano hayo ya Urembo ya Redd’s Miss Tanzania 2012 yanaendelea kwa kasi na kwa wiki hii kutakuwa na shindano moja ambapo kituo cha Ubungo yaani “REDD’S MISS UBUNGO 2012” kitakuwa kikifanya shindano lake.

Shindano hili litafanyika siku ya Ijumaa tarehe 29 / 06 / 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya LANDMARK iliyopo ubungo kuanzia saa mbili usiku.

kiingilio katika shindano hili kimepangwa kuwa Tsh. 10,000/= kwa upande wa burudani itakayosindikiza shindano hili itatoka kwa bendi ya FM ACADEMIA (wazee wa ngwasuma)

kituo hiki cha miss ubungo ndicho kilichomtoa Miss Tanzania 2004 FARAJA KOTTA, hivyo ni mategemeo yetu tutatoa tena Miss Kinondoni na hatimae ndie atakaekuwa REDD’S MISS TANZANIA 2012.

na warembo watakao chuana katika kinyang’anyiro hicho ni ASHA MUSA (20), FOTUNE ANDE (22),MWATUMU MUSTAPHA (21),ZAWADI GULABA (18), LILIAN KENNEDY (21), DALINE MMALY (19), AXER PETER (20), NASRA DAFFA (22), JOYCE RAPHAEL (20),PRINCES REMMY (20), MWANAIDI RAMADHANI (20), ZENA ALLY (18), DORICE CHILONGOLA (20),SUZAN STANLEY (21),ADAIYA AHMED (22) na SAHY PAUL (22)

.