Makundi mbalimbali ya wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya kitaifa wakiwa katika mafunzo kwa njia ya vitendo jana katika Kijiji cha Nala mkoani Dodoma jinsi ya kutumia ramani katika zoezi la sensa ya watu ambayo inatarajia kufanyika nchini kote tarehe 26.08.2012. Wakufunzi hao wako mkoani Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya kuwawezesha ili nao waende kutoa elimu hiyo katika ngazi za mikoa.