Sekondari Tosamaganga Iringa kwachafuka mabomu

Wanafunzi wa Sekondari ya Tosamaganga wakikimbia moshi ya mabomu yaliyokuwa yakipigwa na polisi.

Polisi wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tosamaganga eneo la Kitwiru nje kidogo na Manispaa ya Iringa hapo ilikuwa ni kabla ya kuanza kupiga na kurusha mabomu ya machozi.Wanafunzi wa Sekondari ya Tosamaganga wakikimbia moshi ya mabomu yaliyokuwa yakipigwa na polisiMwandishi wa habari wa radio Ebony Fm akikimbia moshi ya mabomu ambayo yalikuwa yakipigwa na askari hao kutawanya wanafunzi hivi pundeHapa wakikimbia porini kunusuru afya zao

Hali ya usalama si shwari katika shule ya sekondari Tosamaganga Wilaya ya Iringa mkoani Iringa jana haikuwa shwari kwani wanafunzi zaidi ya 1000 walikimbilia porini wakikimbizwa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ambao wanatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa katika maandamano ya amani kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuulalamikia uongozi wa shule hiyo.

mabomu zaidi ya 10 ya machozi yalipigwa kuwatawanya wanafunzi hao ambao baadhi yao walidaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na miti wakati wakikimbia porini kukwepa mabomu huku wananchi wa Mseke nao wakikimbia nyumba zao kujinusuru na mabomu.

Polisi waliwazuia waandishi wa habari akiwemo Mwanalibeneke Mpiganaji wa Globu ya www.francisgodwin.blogspot.com pamoja na Globu ya Jamii ambao waliokuwepo eneo hilo wakifuatilia tukio hilo kuendelea kuchukua habari hiyo.