NA MWANDISHI WETU SHINYANGA
MENEJA UENDESHAJI WA SHIRIKA LA KUHUDUMIA WALEMAVU WA NGOZI NCHINI, GAMAREL MBOYA AKIWAVISHA KOFIA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI KATIKA SHULE MAALUM YA BUHANGIJA MANSPAA YA SHINYANGA SIKU YA MTOTO WA AFRICA.
AKIZUNGUMZA JANA MJINI HAPA BAADA YA KUKABIDHI MISAADA MBALIMBALI IKIWEMO KOFIA,NGUO PAMOJA NA NDOO MENEJA HUYO AMESEMA TATIZO LILILOPO HIVI SASA KATIKA SHULE NYINGI AMBAZO WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI WANASOMESHWA NA SHIRIKA LAKE NI KUTENGWA NA WAZAZI WAO
AMESEMA KUWA TANGU WATOTO HAO WACHUKULIWA NA KUSOMESHWA IKIWA PAMOJA NA WALE WA SHULE MAALUMU YA BUHANGIJA WAMETENGWA NA WAZAZI WAO KWANI AKUNA MZAZI ANAYEJITOKEZA KUWAONA WATOTO HAO
AMESEMA HALI HIYO INASABABISHA WATOTO HAO KUKOSA UPENDO WA FAMILIA PAMOJA NA KUWA NA MZIGO MKUBWA KWA SHIRIKA LAKE PAMOJA NA SERIKALI KUWAHUDUMIA MAMBO MBALIMBALI
AMESEMA WAZAZI WANAWAJIBU WA KUWAONA WATOTO WAO NA KUWAPA MAHITAJI MBALIMBALI KWANI SHIRIKA LAKE LINAWASOMESHA TU NA KWAMBA NI VYEMA JAMII IKATAMBUA HILO