KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ameahidi kuwapa vifaa vya michezo timu za vijana wanaojishughulisha na kazi za ujasiriamali eneo la Kituo cha mabasi cha mjini Mafinga, katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Katika ahadi hiyo Nape amesema atatoa mipira sita na jezi kwa timu nne za vijana wanaojishughulisha na kazi hizo ambazo ni pamoja na wakatisha tiketi, madereva wa teksi, pikipiki, na biashara ndogo ndogo katika eneo hilo la stendi.
Nape alitoa ahadi hiyo jana, baada ya kuzindua shina la wakereketwa wa CCM, wajasiriamali wanaofanya shughuli mbalimbali kwenye stendi hiyo ya mabasi.
Pamoja na kuahidi kutia vifaa vya michezo, Nape aliahidi pia kuwapa vijanwa shina hilko kianzio cha sh. milioni moja kwa ajili ya kufungua akaunti benki, ili shina hilo, liwe la watu wanaojishughulisha na kazi badala ya kuwa kijiwe cha kupiga soga.
“Katika maamuzi yetu ndani ya Chama, CCM imeamua kwamba matawi na mashina ya watekereketwa wetu, sasa yanedne mbele zaidi, badala ya kuwa ya shughuli za siasa lakini yawe vituo vya kuktanaia wazalishaji mali na shughuli ngingine za maendeleo”, alisema Nape.
Akijibu risala iliyosomwa na uongozi wa shina hilo, Nape aliagiza uongozi wa wilaya, kuhakikisha unaismamia mamlaka zinazohusika ili maji yaweze kupatikana kwenye eneo hilo la stendi kwa sababu kuna mahitaji makubwa ya matumizi ya maji ili kipafanya pawe mahala pazuri kwa shughuli za wasafiri na wafanyabiashara eneo hilo.
“Mkuu wa wilaya, nakuagiza ukae haraka na Baraza la madiwani la hapa, ili mhakikishe maji yanafika napema enei hili kwa sababu watu hawa hawawezi kuendelea na shughuli zao hapa wakiwa hawana maji, wakati uwezekano wa kuyafikisha hapa upo”, alisema.
Mapema katika risala yao, viongozi wa shina hilo, walisema, ene hilo la stebdi linapaswa kuwa na maji kwa kuwa kutokuwepo huduma hiyo kutasababisha pachafuke haraka na hivyo kutokuwa mahali bora kwa shughuli mbali mbali na pia hatari kwa afya za watu.
Nape alikuw wilayani Mufundi akiwa katika ziara ya siku nne mkoani Iringa kukagua uhai wa Chama na kuhimiza maendeleo.