NATO imeshambulia nyumba ya Gaddafi

Muammar Gaddafi

TAARIFA kutoka katika Jeshi la NATO zinaeleza vikosi vya jeshi hilo vimeangamiza minara ya walinzi katika eneo la nyumba ya Kanali Muammar Gaddafi wa Libya mjini Tripoli.Imeelezwa kwamba yamefanyika mashambulio mawili yaliyofanywa na ndege za umoja huo wa kijeshi.

Waandishi wa habari mjini Tripoli, wanasema shambulio moja lilofanywa mchana, lilivunja sehemu za ukuta unaozunguka jengo la jeshi la Bab al-Aziziya.

Hata hivyo mmoja wa wasemaji wa NATO, alieleza kuwa shambulio hilo ni funzo kubwa kwa kiongozi wa Libya, kwamba hawezi tena kujificha nyuma ya kuta ndefu.