Shule ya msingi Etaro na kilio cha madawati

wanafunzi wa shule ya msingi Etaro wakiwa darasani

Uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari umeendelea kuumiza vichwa vya wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla nchini.

Hii ikiwa ni pamoja na upungufu wa madawati katika shule za msingi unaoendelea kudidimiza kiwango cha elimu nchini huku ukichangia kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha wanafunzi wengine kukata tamaa ya kusoma na mazingira ya shule kwa ujumla ambayo si rafiki kwao.

Matokeo ya wanafunzi kukaa chini husababisha wanafunzi kuandika wakiwa wameinama na wengine hata kulala kifudi fudi na wengine kuchuchumaa na hivyo kushindwa kuandika vizuri na pia kuchoka mapema.Hali hii kupelekea matokeo mabaya nyakati za mitihani hasa ya kitaifa.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Etaro wakiwa darasani wakimfuatilia mwalimu.wanafunzi wengi katika shule hii wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati.