JK akutana na Wabunge wa EA

Rais Jakaya akizungumza na wabunge watakao iwakilisha Tanzania katika bunge la A.Mashariki

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho kikwete, amekutana na Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashari kijijini Arusha.
Mhe.Rais, ambaye aliwakaribishaWabunge hao kwa chakula cha mchana katika hoteliya Ngurdoto Mountain Lodge, aliwapongeza kwakuchaguliwa kwao kuiwakilisha Tanzania katika Bunge hilo la Jumuiya, na kuwataka wasimamie na kutetea maslahi ya nchi wakiwa huko.
Pia Rais amewataka Wabunge hao kuwakaribu na Serikali katika kushauriana namna ya kukabiliana na changamoto zitazojitokeza katika kazi zao, nakuwakumbusha kwamba majukumu ya Bunge hilo la Jumuiya nikusimamia makubaliano (treaty) yaliyoyo orodheshwa katika kuundwa kwake na kuendeshwa.
Alisema: “Msome vyema na kuyaelewa makubaliano (treaty) hayo yote na vipengele vyake na msaidie kuiendeleza Jumuiya ambayo wanachama wote watanufaika nayo, na siyo upande mmoja.
“Tumewapeleka pale kwa ajili ya maslahi ya Tanzania hivyo mjue kuna kazi nyingi kweli, hasakatikakujadiliyaleyoteyaliyokubaliwakatikamakubalianoyajumuiya” alisema.
Rais alikutana na Wabung ewote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki isipokuwa mmoja, Bi. Nderkindo Perpetua Kessy ambaye hakufika kwasababu iliyoelezwa kuwa nimgonjwa.
Waliofikani pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Shy-Rose Saddrudin Bhanji.
Wengine waliofikani Anjela Charless Kizigha, Maryam Ussi Yahya, Dkt Twaha IssaTaslima, Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Bernard Musomi Murunya na Charles Makongoro Nyerere.
Wabunge hao wanatarajiwa kuungana na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi Juni 5, 2012 katika kikao chao rasmi cha kwanza ambapo watamchagua Spika na kisha kula viapo kabla ya kuanza majukumu yao.