Malkia ahitimisha sherehe za miaka 60

ZAIDI ya watu milioni moja waliohimili mvua kali wameshuhudia msafara wa Malkia wa takriban mashua 1,000 wakati wa kuadhimisha miaka 60 ya utawala wake kupitia mto Thames.
Mashua ya Malkia ilikua katikati ya msafara wa mashua za aina mbalimbali, zinazotumia nishati ya mvuke, za kupiga kasia, mashua za kifahari, kayak na mjengo wa Kichina maarufu kama Dragon.
Shughuli hii ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya utawala wa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza.
Takriban watu 10,000 wqalishiriki tafrija ya mitaani huko Greenwich, mojapo ya vitongoji vya jiji la London ikiwa ni mojapo ya tafrija nyingi zilizofanyika kote nchini Uingereza kuadhimisha miaka 60 ya utawala wa Malkia.
Shughuli ya mtoni Thames ilianza rasmi kwa kengele za miaka 60 ya utawala ilipotimu saa nane na dakika 40 saa za Uingereza na zilipangwa kumalizika kwa mashua ya mwisho kuvuka daraja la Tower baada ya safari iliyoanzia kwenye daraja la Albert magharibi mwa mji.
Malkia akivalia kofia nyeupe na koti yenye rangi ya fedha iliyochanganya nyeupe iliyoshonwa na Angela Kelly, alipelekwa kwenye mashua mwanzoni mwa safari kuzindua mashua ya anasa Royal Yacht Britannia na baada ya kusalimiwa kwa wimbo wa Taifa ulioimbwa na ummati wa watu waliokuja kushuhudia sherehe.
Wakati wote Malkia alisindikizwa na wana wa Ufalme wakuu, akiwemo Duke wa Edinburgh(Mumewe) pamoja na Duke na Duchess wa Cambridge, kwenye mashua yao, iliyopambwa mauwa 10,000 kutoka mashamba ya makaazi ya Kifalme.
Hadi watu 20,000 walikisiwa kua kwenye mashua zilizosafiri leo kwa mwendo wa kasi ndogo ya bahari ya maili nne na nusu kwa kila saa. Wakati wote huo kizuizi cha Mto Thames kilibanwa ili kupunguza kasi ya maji ya Mto.
Shangwe na makofi yalipigwa kila sehemu mashua ya Kifalme ilipoonekana. Baada ya siku yenye kivuli ilimiminika mvua kali lakini haikuonekana kuvunja nyoyo za watu waliofurahia siku hii.

-BBC