NMB yatoa mafunzo kwa vyama vya ushirika Tarime

NMB yatoa mafunzo kwa vyama vya ushirika Tarime

Na mwandishi wetu
Tarime,

BENKI ya NMB tawi la Tarime imeendesha mafunzo kwa vyama vya msingi vya ushirika yanayohusu namna ya kutumia stakabadhi ya mazao ghalani katika maandalizi ya ununuzi wa zao la kahawa katika msimu mpyaunaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Katibu tarafa wa Kata ya Inchage Machango Jonathani alisema hiyo ni fursa pekee kutoka katiuka benki hiyo katika kuwapa mafunzo viongozi hao kabla ya kuingia katika msimu wa manunuzi ya zao hilo na kuwataka kwenda kueneza elimu hiyo kwa wakulima mashambani.

Alisema mfumo huo wa stakabadhi ya mazao ghalani unaotumiwa na benki ya NMB unamuwezesha mkulima kuuza mazao yake kwa bei iliyo nzuri na kupata malipo yake bila kuzungushwa hivyo wakulima wakifikishiwa taarifa zilizo nzuri watautumia mfumo huo.

Meneja wa kanda wa mfumo wa mazao ghalani wa benki ya NMB Samwel Msote alisema wameamua kuyatoa mafunzo hayo mapema ili kuwajengea uwezo viongozi hao wa vyama vya msingi vya ushirika Wilayani Tarime ili kuwepo na ufanisi zaidi katika ununuzi wa msimu huu na kuvuka lengo.

Alisema katika msimu wa mwaka jana licha ya kutengwa fedhs nyingi kwa ajili ya mfumo huo vipo vyama vya ushirika ambavyo vilishindwa kuzitumia kwa kufanya manunuzi huku vingine vikifanya manunuzi kidogo ya kahawa na kuwataka viongozi hao kujipanga mapema hili msimu huu vyama hivyo viweze kununua zao hilo kwa wingi.

Alkidai kahawa ya Tarime katika msimu uliopita ilikuwa nzuri na yenye ubora na kupitishwa na bodi ya kahawa Tanzania na kuwaomba viongozi hao kuendela kuwahamasishwa wakulima jinsi ya utunzaji wa zao hilo hili liweze kupata ubora zaidi.

Kwa upande wak meneja wa benki ya NMB tawi la Tarime Amosi Daniel aliwataka viongozi hao wa vyama vya ushirika kufungua accaunti ya busines accaunti kwani ndio accaunti pekee inayotumika katika malipo ya stakabadhi ya mazo ghalani na kuwataka kuwa makini katika uandikaji wa Hundi za malipo.

Naye Katibu wa chama cha ushirika cha Bungerere Lucas Masa alisema huo ni mfumo mzuri unaoendeshwa na benki hiyo ya NMB kwa kuwa unamuwezesha mkulima kuweka mazao ya ke ghalani na kupata mkopo ambao unamuwezesha kutatua matatizo mbalimbali na kuharakisha shugfhuli za maendeleo.

Aidha katibu huyo aliiomba Serikali kwa kupitia maafisa ugani kuhakikisha wanafika kwa wakulima vijijini na kuwa na ushirikiano wa karibu na vyama vya ushirika ili kuweza kubolesha zao la kahawa kwa kuwa tayari Wananchi wa Tarime wameshapata mwitikio mkubwa juu ya zao hilo.