Afya ya uzazi kupewa kipaumbele mchakato wa Katiba mpya

mama akimnyonyesha mtoto wake katika hospitali ya mwananyamala

JAMII iimeshauriwa kulipa kipaumbele suala ya mapendekezo ya kuwepo kwa sheria ya Afya ya Uzazi Salama katika mchakato wa kuwepo kwa Katiba Mpya , ambayo itawezesha watumishi wa afya ambao watasababisha vifo vya wakinamama wajawazito au watoto wachanga kwa sababu za uzembe.
Kauli hiyo iliyoilitolewa leo (jana) na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA), Tike Mwampipile, wakati akifafanua ya mapendekezo hayo iliyoandaliwa na chama hicho kwa waandishi wa habari kwenye semina ya siku mbili iliyofanyika , Ubungo Plaza jijiini Dares Salaam.Semina ya mafunzo hayo ambayo iliyoanza jana (juzi) na kumalizika leo(jana)
“ Wito wangu katika jamii ni ni ina wajikubu mkubwa wa kujua haki zao za msingi na kufahamu wapi pa kuzipata. Afya ya Uzazi Salama ni kitu muhimu ambacho hakijangaliwa kwa umakini. Hivyo katika mchakato wa Katiba Mpya suala hili liangaliwe kwa uzito kwa na upana wake kujali mama ambaye analemta mtoto hapa duniani ambaye anaweza kuwa na Rais au Waziri Mkuu wa kesho,” alisema Mwampipile.
Aliongeza kuwa kuwepo kwa sheria hiyo kutasaidia kupunguza idadi ya vifo vya wakinamama wajawazitio na watoto wachanga.
Kwa upande wake mtoa mada wa mapendekezo hayo, Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya TAWLA na Wakili wa Kujitegemea alisema kuwa mwanamke ana haki ya kuishi na kulindwa ,hivyo sheria hiyo italuiwezesha taifa kupata watoto waliolelewa katika mazingira bora na afya njema. .
“ Tunataka tuwe na sheria ya iyatomlinda mwanamke wakati wa ujauzito na siku 42 baada ya kujifungua,” ikiwepo kupanga idadi ya watoto atakaoweza kuwalea na muda wa kupata mtoto mmoja baada ya mwingine alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu sheria hiyo alisema itamwezesha mamamjamzito kupata huduma za afya ya uzazi salama bora na ambazo zitamwezesha kupata vifaa tiba vinavyotakiwa bila gharama yeyote.
Aidha Mkandya aliongeza katika sheria hiyo wamapendekeza kuwa umri wa uti mzima uwe ni miaka 18 ili kuwezesha mtoto wa kike kuolewa katika umri unaotakiwa hatua ambayo itasaidia kupunguza athari za afya ya uzazi zinazotokana na umri mdogo. Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa makundi yote katika jamii kushiriki katika kutoa maoni ya mchakato huo.
Mkandya aliongeza kuwa mapendekezo hayo hayo yanaelekeza kuwepo kwa sheria ambayo itamwezesha mama mjamzito kusitisha ujauzito pale itakapogundulika kuwa unasabbaisha athari za kiafya kwa ruhusa ya daktari na ridhaa yake au endapo atakuwa amebakwa na kwa ridhaa yake kuwa hana uwezo wa kuendelea hudumia ujauzito huo na kumlea mtoto pale atakapojifungua.
Pia ridhaa hiyo inaweza kutolewa na ndugu zake endapo mama huyo ni mlemavu wa akili .