TAWLA yatoa semina ya Katiba kwa Waandishi wa Habari

Wakili Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA akizungumza katika semina ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali iliyoandaliwa na TAWLA inayozungumzia Mabadiliko ya Katiba na haki ya Afya ya Uzazi inayofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pear Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.


Moja ya mada zilizochukuwa muda mrefu kujadiliwa ni ile ya Katiba Mpya, ambapo wajumbe walitaka iweke wazi kuwa haki ya mtoto wa kike atambulike ni mtu mzima akiwa na miaka 18 na si vinginevyo pia izungumze wazi juu ya elimu ya mtoto wa kike, kuwa angalau apate elimu kufikia kidato cha nne. Pia washiriki wanapendelea kuwa katika katiba iundwe tume ya kushughulikia masuala ya jinsia ya Mwanamke na mwanaume.

Wakili Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA aakifafanua jambo katika semina hiyo.