Na Shomari Binda, wa Binda News-Musoma
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Musoma lililokuwa na ajenda 9 limeendeshwa kwa dakika 10 huku madiwani wa kambi ya Upinzani wakilalamika kuwa wingi wa madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unachangia balaza hilo kuendeshwa kwa ubabaishaji.
Akizungumza na mwandishi mara baada ya kikao hicho, Diwani wa Kata ya Kiriba kupitia Chama cha APPT-Maendeleo Malinda Mafuru alisema licha ya kuwa na umuhimu wa Baraza hilo Madiwani wanaotokana na Chama cha Mapinduzi walipitisha ajenda za kikao hicho kwa kusema ndio kwa kila Ajenda kutokana na wingi wao hali iliyopelekea kushindwa kwa kujadiliwa kwa kina kwa masuala muhimu.
Diwani huyo alisema uendeshwaji wa vikao wa stahili hiyo unashindwa kuwatendea haki Wananchi kwa kuwa Madiwani wapo katika Baraza kwa kuwawakilisha na kushindwa kuzungumzia hopja kwa kina kutokana na wingi wa uwakilishi si jambo la busara na kuwataka Madiwani wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) wabadilike na kuwatendea haki wananchi.
“Haiwezekani kikao kina zaidi ya karatasi 500 za kujadili alafu kinaendeshwa kwa dakika 10 hii haiwezekani tuache habari za kisiasa na tuwatendee Wananchi haki hawa wenzetu licha ya wingi wao wa uwakilishi si kila jambo kusema ndio hata katika yale yenye maslahi kwa Wananchi na Taifa.
“Nadhani ifike mahala Wapiga kura wawe wakali na wanatakiwa wawe wanahudhulia katika mabaraza hili waonapo uozo huu ukifika wakati wa Uchaguzi wachague Madiwani wengi wa Upinzani ili uwakilishi uwe mkubwa na kukomesha masuala ya kusema ndio kwa kila jambo na kushindwa kujadili kwa kina masuala ya msingi.” alisema Malinda.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bukima kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Mayamba Mgeta alisema kulikuwa na hoja muhimu kama kujibu hoja za ukaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) lakini hawa Madiwani wa (CCM) wanashindwa kuelewa umuhimu wake na kupitisha pasipo kujadili kwa pamoja kwa madai kuwa tayari wameshajadili katika vikao vya Chama.
Alisema licha ya ajenda hiyo kuklikuwa na suala lingine la kutoa taarifa ya wajumbe walioteuliwa katika Kamati ya Ardhi ambayo wao walikuwa na sababu ya kuipinga kupitia Baraza hilo kutokana na kuteuliwa kwa madiwani wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pekee lakini walishindwa kufanya hivyo baada ya kupitishwa kwa kura za kusema ndio baada ya kushindwa kutokana na uchache wa uwakilishi wao.
“Huku ni kuburuzana na hali hii itafikia mwisho kwa kuwa Wananchi wa sasa wanaelewa madhara ya kuwachagua wawikilishi wengi wanaotokana na Chama kimoja na naamini katika Chaguzi zinazokuja watahadhibiwa kutokana na haya wanayoyafanya ya kutowatendea haki Wananchi waliowapoa uwakilishi,” alisema Mayamba.
Alisema hata kama ajenda zililetwa katika vikao vya chama lakini baraza lina umuhimu wake kwani kuna Wananchi amabo wanahudhulia katika vikao vya baraza ambao hawana nafasi ya kufika katika vikao vya Chama wanapaswa kusikiliza na kuelewa kila kitu kinachohusiana na Baraza la Madiwa na hoja zinazojadiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Magina Magesa (CCM) alisema ajenda zote zilizoletwa katika Baraza hilo tayari zilishapekwa katika vikao vya Chama na kupata nafasi za kujadiliwa kwa muda mrefu hivyoi baraza hili lilikuwa na kazi ndogo ya kuzithibitisha.