Ajali mbaya Babati, watu 6 wafa wawili majeruhi

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Said Mwema

Na Mwandishi Wetu, Thehabari-Manyara

HABARI zilizotufikia zinasema watu sita (6) wamefariki dunia huku wengine wawili (2) wakijeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Sigino wilayani Babati mkoani hapa baada ya gari hilo kufeli breki na kuanguka. Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Akili Mpwapwa alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei25 mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi.

Kamanda Mpwapwa alisema kuwa gari aina ya Scania lililokuwa na namba za usajili T 536 AGJ likiwa tela namba T 575 BHJ lilikuwa limebeba mbao likisafirisha kutoka mkoani Iringa kuelekea Wilaya ya Babati.

Alisema kuwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ambayo imetokea katika eneo lenye mteremko mkali na pale gari gari hilo lilipoanguka baada ya dereva wake kushindwa kulimudu lilipokuwa linaserereka katika mteremko wa Sigino mara baada ya breki zake kufeli.

alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja lilikuwa na watu wengine watano(5) ambao wote walifariki papo hapo.

Alisema kuwa majeruhi hao walikuwa ni watembea kwa miguu katika eneo hilo na wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Babati ya Mrara kwa matibabu zaidi.

Mpwapwa alisema majina ya waliofariki hayajaweza kufahamika mara moja na uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea huku miili ya marehemu ikiwa imehifadhiwa katika hospitali hiyo ya Wilaya pia. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo ni Paulo Charles (38) wa Mafinga, Iringa wengine ni mmiliki wa gari hilo amefahamika kwa jina la Josephat Mkalama ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Babati. Hata hivyo majina ya wengine hayakuweza kufahamika mara moja.
Mtandao huu utaendelea kuwajuza taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo