Makala kutatua mgogoro wa ardhi kinyenze

mbunge wa mvomelo Makala akijadiliana na wananchi wa Kanyenze

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( aliyesimama na kunyosha mkono juu) akisisitiza jambo juu ya namna ya kutafuta muakafa ili kumalizwa kwa mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kitongoji cha Kinyenzi dhidi ya Mwekezaji wa kizungu.(Picha kwa Hisani ya FATHER KIDEVU BLOG)

wananchi wa kijiji cha kanyenze wakipata ufafanuzi toka kwa afisa ardhi wa Wilaya yao

Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jafari ( aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa mgogoro wa shamba namba shamba 296 kati ya wanachi wa Kitongoji cha Kinyenze na Mwekezaji wa Kizungu kwenye mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo , uliofanyika hivi karibini ( Mei 19) uliokuwa na lengo la kufikia utatuzi wa mgogoro huo(Picha kwa Hisani ya FATHER KIDEVU BLOG)

wanakijiji wakifatilia mjadala kwa karibu

Baadhi ya wazee na wananchi wa Kitogoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera,Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla ( hayupo pichani) wakati akipowatembelea hivi karibuni ( Mei 19) wananchi wa Kitongoji hicho kwa ajili ya kupanga mkakati wa kumalizwa mgogoro kati ya mwekezaji wa kizungu na wakazi hao, Mbunge huyo pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo. (Picha kwa Hisani ya FATHER KIDEVU BLOG)