Hashim Lundenga aliwataka warembo hao kujiheshimu maana urembo ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na warembo wengi wanaojiheshimu na kuwa na tabia njema katika jamii huwa na mafanikio makubwa.
Wakati Nameems Wear wakiwa ni wadhamini wakuu, wakisaidiwa na Reds, Dodoma wine, Clouds FM, Lady Pepeta, Father Kidevu Blog, Jambo Leo, Aucland Tours & Safaris, Candy Bureau de Change, Flexip, PJ Amusement, Renzo Salon na Madishisha Video Production.
Aidha Jumla ya warembo 16 wamejitokeza kuwania taji la Redds Miss kurasini 2012, ambalo taji linashikiliwa na Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma.
Akiwataja warembo waliopo kambini na kunolewa na Mwajabu Juma akisaidiwa na Malkia wa vipaji wa Miss Tanzania 2011, Rose Hurbert ni Mariam Sadic (19), Johari Juma (20), Linda Deus (20), Irene Sostheness 20), Neemadoree Sylvery(29), Edna Magige (22), Lindanancy Joseph(20), Elizabeth Mkende (19), Betty Peter (22), Jennifer Njabili (18), Lilian Joseph (20), Farida Mrope (23),Christina Moses (20), Angle Gasper (19), Flaviana Maeda(22) na Sia Kimambo (19).