MABONDIA, Ramadhan Kumbele na James Mokiwa wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho katika Ukumbi wa VIJANA – KINONDONI. Mabondia wote wapo katika hali nzuri na wamejinadi kila mmoja kushinda.
Katika mpambano huo ambao utakuwa wa Ubingwa wa Bantam weight (53.5kgs), ubingwa wa taifa utakaosimamiwa na TPBO. Imeelezwa kuwa pambano hilo litatanguliwa na mapambano ya kadhaa ya utangulizi, likiwemo la Jafar Majia na Daud Muhunzi la raundi sita, Mustafa Doto na Amos Mwamakula la raundi sita (feather weight), Doi Miyeyusho atacheza na Jumanne Mtengela raundi sita.
Mapambano mengine ni middle weight, kati ya Francis suba na Ibrahim Tampa raundi sita, fly weight, Sadat Miyeyusho atacheza na Swedi Hassan, Martin Richard na Yohana Thobias.
Bigright Promotion wamejipanga vema kuhakikisha mapambano yanakwenda vizuri kama yalivyopangwa na ulinzi wa uhakika wakati wote wa burudani. Muziki toka kwa Karapina pamoja na show za mabondia wadogo pia zitakuwepo.