Wananchi wamtaka Mbunge wa CCM ahamie CHADEMA

Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Muhagama

*Ni Ester Bulaya mbunge wa Viti Maalumu

Na Shomari Binda Musoma, Wa Binda News

MBUNGE wa Viti Maalumu mkoani Mara kupitia vijana (CCM), Ester Bulaya amehututubia mkutano mkubwa katika Uwanja wa Sabasaba mjini Bunda uliohudhuliwa na maelfu ya Wananchi, huku baadhi wakimtaka mbunge huyo kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Katika mkutano huo ambao inadaiwa kuwa ni mkutano ambao haujawahi kufanywa hata na Mbunge wa jimbo hilo, Stiven Wasira tangu amechaguliwa, Bulaya aliwataka vijana kushiriki kwa asilimia kubwa katika mchakato wa Katiba Mpya.

Akihutubia katika mkutano huo Bulaya alisema hakuna suala la muhimu kama Katiba katika kipindi hiki kwa kuwa ndio itakayotoa muelekeo wa maisha na kuwakomboa katika masuala mbalimbali ikiweo Elimu,afya na shughuli za kimaendeleo katika kujikwamua kuondokana na umasikini.

Alisema ni muhimu kujitokeza katika hatua zote za mchakato wa Katiba na kutoa maoni kwa kila hitaji ili kuweza kuondoa malalamiko mbalimbali ambayo yamekuwa yakielezwa katika katiba iliyopo na kuwahimiza hususani vijana kuchulia umuhimu wa kipekee suala hilo kwa kuwa wao ndio wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika jambo hilo na kuwahamasisha wengine.

“Ndugu zangu vijana wenzangu,nyie pamoja na mimi ndio msingi mkubwa wa kuchukulia umuhimu wake suala la katiba mpya ambayo mchakato wake umeanza kuanzia mei mosi naomba tushiriki kwa kila hatua maana nchi hii kuna masuala mengi ambayo bila kuyapigania kupitia katiba mpya hatutaweza kufanikiwa kamwe.

“Nchi hii habari mbalimbali za kifisadi zimeelezwa na kutangazwa na vyombo mbalimbali vya habari lakini tunashuhudia hakuna hatua makini ambazo zimechukuliwa lakini tukitaka kwenye katiba mpya kiingizwe kipengere ambacho kitawabana na kuwachukulia hatua kali mafisadi wote wataogopa na kuacha kufoji mali za umma,”alisema Bulaya.

Alisema wametangazwa viongozi mbalimbali katika sekta za Umma ambao wamejiingiza katika mikataba mibovu ambayo imeendelea kuwafanya Wananchi kuwa masikini licha ya rasilimali walizonazo lakini kushaghulikiwa kwao kumekuwa hakupewi umuhimu wa pekee na kuendelea kukumbatiwa na kusema mkombozi pekee ni kulipa umuhimu wa pekee zoezi a mchakato wa katiba mpya.

Bulaya aliwaomba Wananchi wa Bunda kujenga utamaduni wa kushiriki katika vikao vya mabaraza ya Madiwani ili kuweza kujua bajeti zinazopangwa katika vikao hivyo zinazohusu maeneo yao na kuwa wafatiliaji katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kuacha tabia ya kupuuzia vikao hivyo kwa kuwa ni muhimu na wanapaswa kushiriki.

Alidai kuwa hivi karibuni alipoudhulia kikao cha ushauri cha Mkoa wa Mara (RCC)katika kupitisha Bajeti ya Mkoa Halimashauri ya Wilaya ya Bunda iliomba maombi maalumu kiasi cha shilingi milioni 95 katika kukamilisha hostel ya wanafunzi katika shule ya sekondari Bunda na milioni 402 katika mchakato wa kupandisha kituo cha afya manyamanyama kuwa hospital ya Wilaya na kuwataka Wananchi kufatilia maombi hayo na mchakato mzima kwa kuwa ni haki yao kufanya hivyo.

Wakiongea na BINDA NEWS mara baada ya mkutano huo kuzungumzia yale yote aliyoyazungumza Mbunge huyo kwa nyakati tofauti wananchi wa jimbo hilo la Bunda walisema kuwa wanamtaka Mbunge huyo wa viti maalumu kuangalia uwezekano wa kuamia katika Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) kwa kuwa sera alizonazo zinapingana na chama alichopo.

Walisema wamekuwa wakimfatilia Mbunge huyo katika vikao vya Bunge na amekuwa akitetea maslahi ya wananchi na kuzungumza nao kila panapo malizika vikao vya Bunge kutuambia kile kinachoendelea na kuhamasisha shughuli za Maendeleo hivyo ni mtu muhimu katika kuchangia maendeleo ya Jimbo la Bunda na Tanzania kwa ujumla.

“Kiu kweli Mbunge Bulaya ni mbunge wa kipekee licha ya ugeni wake katika Bunge,amekuwa akitoa hoja zenye kuleta matumaini na amekuwa nasisi mara kwa mara tofauti na wabunge wengine na Chama ambacho sera zake zinzendana ni (CHADEMA) tumuhitajia katika uchaguzi wa mwaka 2015 wakimuwekea zengwe kwenye chama chake aje (CHADEMA),” alisema Musa Wankaba mkazi wa Balili.

Walisema hata mkutano ambao ameufanya unadhilisha ni jinsi gani vijana na Wananchi wa Bunda wanamkubali kutokana na umati uliojitokeza kwa kuwa ni mwajibikaji na anajituma katika majukumu yake akiwa Mbunge wa kupitia vijana.