Mchujo wa kwanza U23 Tanzania na Nigeria Juni 5

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Boniface Wambura, Ofisa Habari wa TFF

Mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya
Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itachezwa Juni
5 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.

Tumepanga muda huo kwa vile uwanja siku hiyo utakuwa unatumika kwa ajili ya
michuano ya riadha ya Kanda ya Tano Afrika ambapo itakuwa inafikia kilele. Kwa
mujibu wa Chama cha Riadha Tanzania (AT) kufikia saa 8 mchana michuano hiyo
itakuwa imemalizika, hivyo kupisha maandalizi ya mechi.

Mechi itachezeshwa na mwamuzi Sylvester Kirwa ambapo atasaidiwa na Peter
Kiereini, Aden Marwa na Davies Omweno wote kutoka Kenya wakati Kamishna wa
mchezo huo atakuwa Sahilu Gebremariam kutoka Ethiopia.