Michango hii Shule ya Msingi Makumbusho inakera

wanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Makumbusho wakiwa darasani

Wanafunzi wa Darasa la Kwanza Shule ya Msingi Makumbusho

LICHA ya Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza kuwa imefuta michango kedekede ya shule za msingi ili kuwawezesha wanafunzi wote kupata elimu bado kuna shule zinaendeleza wingi la michango hiyo.

Waweza kutafakari kwa kuangalia orodha ya michango wanayodaiwa wanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Makumbusho. Mwanafunzi wa darasa la kwanza hutakiwa kulipa kila mwezi sh. 1000 ya mtihani, sh. 1500 mtihani wa muhula, sh. 500 ya uji kwa kila siku, michango ya Tuisheni, Usafi, mchango wa ulinzi, nembo ya shule, kulipia vidumu, fagio pamoja na madaftari ambayo hulazimishwa kununua shuleni hapo na si kwingineko.

Licha ya michango hiyo wanafunzi hao hukaa kwa kushongamana darasani kutokana na wingi wao. Duh! Hii ni changamoto, sijui wanawezaje kusoma kiufasaha.