Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Narita Mjini Tokyo kwa ziara ya siku 6 kwa Mwaliko wa Kikazi kutoka Bunge la Japan. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania, Salome Sijaona. Spika Makinda katika ziara hiyo ameongozana na Ujumbe wa Wabunge 5 kutoka Bunge la Tanzania. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge la Tanzania.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Spika wa Tanzania, Anne Makinda wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meya wa Mji wa Natori, Takamoto Ohta (Kulia) mara baada ya kuweka shada la Maua katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya wahanga wa Mafuriko ya Tsunami yaliyoikumba nchi ya Japan Mwezi Machi mwaka jana alipotembelea Mji wa NATORI, Uliopo Mkoa wa MIAGA ikiwa ni mojawapo ya miji iliyokumbwa na mafuriko Mwaka jana. Spika na ujumbe wa wabunge watano wapo katika ziara nchini Japan kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japan. Kushoto ni Tundu Lissu, Anne Makinda, Rukia Ahmed, James Lembeli, Anne Kilango Malecela, Naibu Meya wa Mji wa Natori, Takamoto Ohta na Godfrey Zambi.