Waziri Mkuu Pinda awasha Mwenge wa Uhuru Mbeya

Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2012 Kepteni Honest Erenest Mwanossa kutoka Dar es Salaam akimkabidhi mwenge wa Uhuru waziri mkuu Mizengo Pinda tayari kwa kuukabidhi kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya tayari kwa kukimbizwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara (Kushoto) akimtambulisha kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2012 Kepteni Honest Erenest Mwanossa kutoka Dar es Salaam (kulia). Picha na Aron Msigwa-MAELEZO

Vijana wa kundi la halaiki kutoka katika shule mbalimbali za mkoa wa Mbeya wakipamba shughuli za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2012 zinazoongozwa na kauli mbiu ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu, Shiriki kuhesabiwa Agosti 26 leo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakiwa wamevaa T-shirt zenye kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi 2012 leo jijini Mbeya wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO