Manispaa ya Musoma kufikishwa Mahakamani

Meya wa manispaa ya Musoma Alex Kisurura akiapa

Na Shomari Binda wa Binda News-Musoma

WANANCHI wa Kata ya Bweri katika eneo la Rwamlimi wamekusudia kuifikisha Mahakamani Halimashauri ya Manispaa ya Musoma kwa kile kilichodaiwa kushidwa kuwalipa fidia ya Aridhi yenye thamani zaidi ya sh. milioni 400 baada ya viwanja vyao kuzuiwa kuendelezwa tangu mwaka 2003.

Wakizungumza na BINDA NEWS Wananchi hao wanaomiliki kaya 36 katika kiwanja namba 868 kitalu ‘U’Mutex wameipelekea Manispaa hiyo notisi ya siku 30 wakitaka kulipwa mchangano wa fidia yao kwa mchanganuo wa kila mmoja la sivyo wataifikisha Mahakamani na kudai gharama za usumbufu waliofanyiwa na Halimashauri hiyo.

Wamesema kuwa wamekuwa na madai yao ya msingi tangu mwaka 2003 baada ya Manispaaa hiyo kufika katika viwanja vyao na kuwazuia kuviendeleza makazi yao kwa kile kilichodaiwa eneo hilo husika lilikusudiwa kuwa uwanja wa michezo na kupimwa kuwa kiwanj namba 868 kitalu ‘U’ na hivyo makazi yao kuathiriwa na zoezi hilo.

Wamedai kuwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo imeshindwa kujali athari zinazowapata kwa kuishi bila kuendelaza makazi yao baada ya kuzuiwa kwa muda mrefu huku wengi wao tayari nyumba zao zikiwa zimebomoka na kuendelea kukaa kimya pamoja na kufatilia kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kufikisha suala hilo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

“Pamoja na uthamini duni uliofanywa miaka mingi iliyopita na sisi kupata mateso ya kuishi katika makazi waliyotuzuia kuyaendeleza bado Manispaa ya Musoma bado haijalipa fidia husika ingawa ni fidia duni ambazo hazikujalia kipindi kilichopita na mali zilizoharibika kabla ya uthamini,

“Tumekuwa tukitumia muda mwingi katika kufanya ufatiliaji kuliko kafanya shughuli za kimaendeleo na kughalimu fedha pamoja na mali nyingine lakini Ofisi ya Mkurugenzi imekuwa ikitoa majibu ya ajabu ya kutokuwa na uhakika wa kutulipa au la,”alisema mmoja wa wadai hao alijitambulisha kwa jina la Charles Matari.

Wamesema hawawezi kuendelea kuvumilia kuishi katika mateso na shida kwa muda usijulikana kwa sababu ya mamuzi ya kuzui kuendelaza makazi yao maamuzi ambayo hayakuzingatia kwamba hata wanyama na viumbe wengine waishio polini huitaji kuboleshewa makazi yao kila inapobidi.

Walisema kuwa kitendo kilichofanywa na Halimashauri ya Manispaa ya Musoma dhidi ya Wananchui hao wa Rwamlimi ni kitendo cha kinyama na ukatili kisichozingatia misingi ya haki na utawala bora na kimevunja haki za Binadamu kama zilivyohainishwa kwenye Ibara ya 24(1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wamedai notisi hiyo ni fursa ya mwisho kwa ajili ya kutekeleza madai yao bila mivutano mikubwa ambayo inaweza kuleta uhasama kwani tayari madai yao yalishapitishwa katika bajeti ya Manispaa hiyo hivyo kuna viongozi ambao kwa utashi wao wanakwamisha malipo hayo.

Timu ya BINDA NEWS ilifanya jitihada za kumtafuta Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Nathan Mshana ili aweze kuzungumzia madai ya Wananchi hao nakuelezwa kuwa nje ya Ofisi lakini mmoja wa Watumishi katika Idara ya Ardhi ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazeti kudai kuwepo kwa madai ya fidia ya Wananchi hao kwa muda mrefu.