BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya “Ngoma Africa Band” a.k.a FFU yenye maskani yake nchini Ujerumani, imetoa salamu za pongezi kwa wanahabari na vyombo vya habari vyote duniani katika sherehe ya siku ya “uhuru wa vyombo vya habari” kila Mai 3, ya kila mwaka. FFU inawapongeza wanahabari na vyombo vyao kwa kazi nzuri na muhimu wanazofanya za kuwapasha habari walimwengu.
“Mchango wa wanahabari katika kila jamii duniani ni sawa na mbolea katika maisha ya kila siku, kwani maisha bila ya habari ni sawa miti bila mizizi, hongereni sana wanahabari na Wanalibeneke wote duniani,” imesema taarifa yao.
FFU wa Ngoma Africa band sasa wanatamba song lao jipya “Uhuru wa habari” wimbo ambao unasikika at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-Africa.com