Ofisa Uhamasishaji Sensa ya Watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Said Amir akiwaonesha waandishi wa habari vitabu vyenye maelezo mbalimbali kuhusiana na sensa ya watu na makazi itakayofanyika kote nchini kuanzia tarehe 26 Augosti mwaka huu. Jumla ya sh. bilioni 141 zitatumika hadi kukamilika kwa zoezi hilo pia hiyo ni Sensa ya tano kufanyika tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Vijana, Dk. Kissui Steven akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe za kuwashwa kwa mwenge wa Uhuru zitakazofanyika mkoani Mbeya Mai 11. Moja ya kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru ni kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika nchini kuanzia Agosti 26 mwaka huu. Kulia ni Ofisa Uhamasishaji Sensa ya Watu na Makazi, Said Amir.
Mratibu wa Sensa ya watu na makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Irenius Ruyobya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa wananchi kujibu kwa ufasaha maswali watakayoulizwa wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika kote nchini kuanzia Agosti 26 mwaka huu. Jumla ya sh. bilioni 141 zitatumika hadi kukamilika kwa zoezi hilo. Picha zote na Anna Nkinda - Maelezo