Waandishi wa habari za mahakamani kupewa mafunzo

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini

Na Shomari Binda, Musoma

MUUNGANO wa vilabu vya Waaandishi wa Habari hapa Nchini (UTPC) inaendesha mafunzo ya ya siku nne kuhusu Uandishi wa Habari za Mahakama kwa Waandishi wa Habari Mkoani Mara ili kuwajengea uwezo wa kuandika Habari hizo kwa umakini bila kuvunja Sheria.

Akitoa ufafanuzi wa umuhimu wa mafunzo kwa Waandishi takribani 20 kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo, Mwanasheria wa (UTPC) na Mwandishi wa Habari mwandamizi Juma Thomas alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuzingatia mambo muhimu kabla ya kuandika Habari hizo za Kimahakama.

Alisema bado kuna makosa ambayo yanaonekana katika Uandishi wa Habari za Mahakama hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kuwapa mwanga zaidi wa kuweza kuziandika Habari hizo pasipo kujiingiza katika matatizo ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa baadhi ya Waandishi.

Alidai kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kuandika Habari za Mahakama kwa kuwa wapo waandishi ambao wameshakutana na matatizo mbalimbali katika Uandishi wa Habari hizo hivyo lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo zaidi Waandishi ili wasiweze kujiingiza katika matatizo ambayo yamekuwa yakijitokeza katika siku za nyuma.

Akitolea mfano mmoja mkufunzi wa mafunzo hayo Juma Thomas alisema sheria ya mwaka 2009 inazuia kuandika ama kupiga picha mwenendo wa kesi inayomuhusu mtoto inayoendelea katika Mahakama kwa kuwa hilo ni kosa kwa mujibu wa Sheria.

“Ninacho waomba ni kufatilia kwa makini mafunzo haya kwani yatawasaidia na kuwajenga katika kuandika Habari za Mahakama na kujiepusha na mahusianao hasi na malalamiko kwa wenye kesi mbalimbali Mahakamani anbayo hayana msingi bali ni kuwajengea mahusiano yasiyo mazuri,” alisema Juma.

Mada mbalimbali zinatarajiwa kutolewa kuhusiana na Uandishi wa Habari za Mahakama katika mafunzo hayo ya siku nne yanayofanyika katka hotel ya Orange Tree.

Chanzo: Binda News