Dk Magufuli ateua wajumbe Bodi ya Mfuko wa Barabara

Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli (Mb)

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Ujenzi nchini Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli (Mb) ameteua wajumbe wanne wa Bodi ya Mfuko wa Barabara kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri, Dk. Magufuli iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango; waziri amefanya uteuzi huo kutokana na uwezo aliopewa kisheria wa Kifungu Na. 5(2) cha Sheria ya Mfuko wa Barabara Na. 11 ya Mwaka 1998.

“Kwa Mujibu wa Kifungu Na. 5(2) cha Sheria ya Mfuko wa Barabara Na. 11 ya Mwaka 1998 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli (Mb.) amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara kwa kipindi cha miaka mitatu kama ifuatavyo,” imesema taarifa hiyo.

Wajumbe walio teuliwa ni pamoja na Ramadhani Khijjah, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Mhandisi Joseph Nyamhanga, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Barabara, Wizara ya Ujenzi, Willigis Oswald Mbogoro, Kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika.

Wengine ni Mhandisi Peter Daudi Chisawilo, Kutoka Tanzania Chamber of Commerce, Indusry & Agriculture, MOROGORO. Imeeleza kuwa uteuzi wa Khijjah na Mhandisi Nyamhanga ni kuanzia tarehe 1 Machi, 2012. Kwa Mbogoro na Mhandisi Chisawilo uteuzi umeanza tarehe 17 Machi, 2012.