RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amefunga rasmi msimu wa uchumaji wa karafuu mwaka 2011/2012 na kusisitiza kuwa uchumaji unamalizika lakini vita dhidi ya magendo ya karafuu vinapaswa viendelee.
Dk. Shein, aliyasema hayo katika ukumbi kiwanda cha makonyo Wawi, Mkoa wa Kusini Pemba wakati alipokuwa na mazugumzo na Kikosi Kazi cha Taifa ( Task Force), na kukipongeza kwa mafaikio ya kihistoria yaliopatikana katika msimu huu.
Katika hotuba yake, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwahimiza wajumbe wa Kikosi Kazi na wananchi wote kuendelea na vita vya kukabiliana na magendo ya karafuu.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio makubwa yaliyokwisha kupatikana katika suala hilo kuna wajibu wa kukaza kamaba kwani kuna taarifa kuwa wapo baadhi ya watu hawajataka kwenda sambamba na matakwa ya serikali.
Aidha, Dk. Shein alisisitiza kuwa katika kukuza zao la karafuu, Srrikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufanya tafiti juu ya kuogeza thamani ya karafuu kabla ya kuziuza nje kwani mafanikio yake yatawasaidia ubora kwa wakulima.
Alieleza kuwa wengi wanaonunua karafuu za Zazibar huwa wanazisarifu na kutoa vitu mbali mbali hivyo ipo haja ya kulenga katika kufanya hivyo hapa hapa nchini kwani hilo linawezekana kwa mashirikiamno ya pamoja.
Alisema kuwa uanzishwaji wa viwanda vya kusindika karafuu ili kutoa mafuta ni hatua mojawapo Shirika la Biashara la Taifa ZSTC kwa hivi sasa linasindika makoyo lakini ikumbukwe kwamba katika miaka ya nyuma, Shirika la Clove Growers Assciation CGA na baadae ZSTC lilitengeneza mafuta ya karafuu.
Kutokana na hatua hiyo, Dk. Shein alisisitiza kufanywa utafiti kwa zao hilo pamoja na mazao mengine ya viungo likiwemo mchaichai, mdalasini, mlangilangi na kulitaka Shirika la ZSTC kubadilika kwa kuwashajiisha wakulima kupanda vitu hivyo.
Alisema kuwa hadi Machi 30 mwaka huu serikali imefanikiwa kununua tani 4749.4 kwa T.shilingi 71 bilioni ikiwa ni sawa na asililimia 158.3 ya lengo lililowekwa la kununua tani 3,000 tu kwa msimu wa mwaka huu ambapo alisema kumemtia moyo nsana.
Alisema kuwa uunuzi wa tani hizo kwa msimu huu ikilingaishwa na tani 2,164 zilizonunuliwa msimu uliopita sawa na ongezeko la asilimkia 119.5 nao umempa imani kuwa inawezekana huu akielez kuwa licha ya kufunga msimu bado karafuu zilizobakia itaendelea kununuliwa na Shirika la ZSTC.
Dk. Shein alieleza kuwa licha bya kuwa karafuu imeshuka thamani katika soko la dunia lakini serikali ya Mapinduzi Zazibar iliendelea kununua bei ile ile iliyowatangazia wananchi na itaendelea kwani haitokula hasara na kusisitiza kuw hadi msimu unamalizika hamna anaeidai serikali.
Aidha, katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa katika mikakati ya kuandaa mikakati ya kuzitafutia karafuu za Zanzibar Hatimiliki na Nembo ya ubora wake (Brand), ni lazima Wizara iweke utaratibu maalum wa kuwaelimisha watu, kw kutumia kitengo vchake cha elimu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuandaa programu maalum.
Dk. Shein alilitaka Shirika la ZSTC kuendeleza mikakati yake ili zao hiloliendelee kuimarika na kuwapa imani zaidi wananchi juu ya zao hilo katika misimu ijayo.
Nae Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazurui alitoa pogezi kwa Rais Dk. Shein na kueleza kuwa mafanikio yaliofikiwa katika kuliimarisha zao hilo zimetokana na juhudi zake
Waziri Mazurui alisema kuwa amefarajika kwa uwamuzi wa kuendelea na kazi Kikundi cha Kikosi Kasi na kueleza kuwa lililobaki hivi sasa ni kuimarisha mikakati kwa misimu ijayo ili kuweze kupatikana mafaikio zaidi.
Alisisitiza kuwa ipo haja ya kuliwekea nembo maalum zao hilo hatua ambayo ianze kwa kila mzanzibari, ila kiongozi, kila nyumba na kila afisi na hata katika sehemu za matangazo barabarani itangazwe karafuu.
Pia, alieleza kuwa Wizara yake itaandaa utaratibu maalum wa kuwapongeza na kuwazawadia wakulima, vikosi vya ulinzi na wafanyakazi wa ZSTC ambao wameshiriki vyema katika uuzaji na ununuzi wa zao hilo msimu huu.
Mapema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Julian Raphael akitoa tathmini ya kazi iliyofanywa na Kikosi Kazi kilichozinduliwa na Dk. Shein katika ukumbi huo huo mnamo Julai 28 mwaka jana kimepata mafanikio makubwa na kutekeleza malengo yake yote yaliowekwa kwa mashirikiano ya pamoja.
Alisema kuwa kumekuwa na mashirikiano makubwa kutoka kwa wananchi pamoja na viogozi wao wakiwemo wakuu wa Mikoa, Wilaya, Masheha na wengineo katika kulilinda zao hilo ambalo hatimae mafanikio yameweza kupatikanwa.
Wizara ya Biashara pamoja na Shirika la ZSTC walimpongeza na kumpa zawadi Dk. Shein ikiwa ni pamoja na kumpa tunzo maalum ya Karafuu ya mwaka 2012 kutokana na mchago wake mkubwa katika mafanikio yaliopatikana katika zao hilo. Rajab Mkasaba Ikulu Zanzibar.