Rais Kikwete akutana na Rais mstaafu wa Brazil, Luis da Silva

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Rais mstaafu wa Brazil, Luis Inancio Lula da Silva alipokwenda kumjulia hali jijini Sao Paulo April 16, 2012. Kushoto ni balozi wa Tanzania nchini Brazil Mh Francis Malambugi na wa pili kushoto ni Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Francisco Carlos Luz

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na na Rais Mstaafu wa Brazil, Luis Inancio Lula da Silva mara baada ya mazungumzo yao alipokwenda kumjulia hali jijini Sao Paulo April 16, 2012.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais Mstaafu wa Brazil Mh Luis Inancio Lula da Silva alipokwenda kumjulia hali jijini Sao Paulo April 16, 2012. (Picha zote na Ikulu)