WAPIGANAJI wa Taliban wameshambulia gereza Kaskazini Magharibi mwa Pakistan, na kuwaachilia huru wafungwa karibu 400.
Polisi wanasema washambuliaji walitumia bunduki na maguruneti katika shambulio hilo jana usiku huko mjini Bannu, karibu na mpaka wa Afghanistan.
Hata hivyo viongozi wa juu wanasema kuwa kati ya wafungwa waliotoroka baada ya kuvunjwa kwa gereza hilo ni wapiganaji na wahalifu wakubwa.
Na kati ya wafungwa waliotoroka ni yumo, Adnan Rasheed, aliyehukumiwa kifo kwa kupanga njama ya kumuuwa rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Musharraf.
-BBC