Muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya Milembe Dk. John Ndimo (Wa tatu kutoka Kulia) akishukuru kwa misaada iliyotolewa na Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma wakati walipotembelea hospitali hiyo jana.
Baadhi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakisikiliza kwa makini maelezo ya Muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya Milembe iliyopo Mkoani Dodoma wakati wanafunzi hao walipofanya ziara.
Ofisa Habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO), Josephat Lukaza akizungumza na Kituo cha ITV wakati wa Ziara ya wanafunzi wa sosholoji walipotembelea hospitali ya Milembe iliyopo Mkoani Dodoma.
Makamu Mwenyekiti Wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma, Gaudensia Mwakemwa akizungumza na kituo cha ITV wakati wa ziara ya Wanafunzi wa Sosholojia wa Chuo Kikuu Cha Dodoma walipotembelea Hospitali ya Milembe jana.