Kabila sasa ataka Ntaganda akamatwe

RAIS wa Congo DRC, Joseph Kabila

RAIS wa Congo DRC, Joseph Kabila amesema kiongozi wa zamani wa waasi, Bosco Ntaganda, anayetafutwa na Mahakama ya Uhalifu ya ICC ni lazima akamatwe. Anasema Jenerali Ntaganda bado yuko nchini DRC. Kabila awali alikataa wito wa kumkamata mtu huyo anayejulikana kama “The Terminator”.

Mahakama ya ICC kwa miaka mitano sasa inamtafuta kwa kusajili watoto kuwa askari wakati wa miaka mitano ya vita vikali DRC. Rais Kabila alifanya mikutano ya dharura na maofisa wa juu wa jeshi mashariki mwa nchi kufuatia mamia ya askari kulikimbia Jeshi la Congo.

Askari wanaomtii Jenerali Gen Ntaganda, walijumuishwa katika jeshi la nchi mwaka 2009. Hata hivyo ndani na kuzunguka Goma ambako majeshi yako wanawalalamikia kuendelea kwa vurugu ikiwemo uporaji na ubakaji tangu kumalizika kwa vita 2003.

“Nataka kumkamata Bosco Ntaganda kwa sababu umati wote wa watu unataka amani. Amefanya uhalifu Kivu ya Kaskazini na Goma…atahukumiwa,” alisema.

Mwezi uliopita mwendesha mashataka mkuu wa ICC alitaka Ntaganda akamatwe mara moja baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani kiongozi mwingine wa waasi, Thomas Lubanga, kwa makosa kama hayo. ICC inasema Jenerali Ntaganda alitumia askari watoto kupigana Ituri kaskazini mashariki mwaCongokuanzia mwaka 2002-2003.

Waasi hao wa zamani haijulikani wako wapi. Inadaiwa kuwa kiongozi huyo aliondoka Goma akiwa pamoja na askari wenye silaha. Baadhi ya taarifa zinasema askari walioasi ni 600 ambao waliambatana naye.

Mchambuzi wa BBC wa masuala ya Afrika Martin Plaut anasema kujitenga huko kunaamnisha wazi kuwakamakutakuwa na majribio ya kumkamata Jenerali Ntaganda kutakuwa na shida baadaye. Msemaji wa jeshi la DRC anasema hatua yoyote ya ukosefu wa nidhamu itakuwa na adhabu yake.

-BBC