Shekh Yahya Hussein afariki dunia Dar

 

Sheikh Yahya Hussein enzi za uhai wake

Na Mwandishi Wetu

Mtabiri maarufu nchini Tanzania, Shekh Yahya Hussein amefariki dunia jijini Dar es Salaam. Mtabiri huyo ambaye huenda amejitabiria kifo hicho amefariki leo osipitalini kwa presha katika Hospitali ya Mkombozi eneo la Moroco Dar es Salaam.

Hivi karibuni mtabiri huyo alitabiri kuwa wafanyabiashara maarufu watatekwa na kushikiliwa hivyo kuwataka wote nchini kuwa makini katika shughuli zao. Hata hivyo kabla ya utabiri huo tayari alikuwa ametabiri kuwa mtu maarufu atakufa, jambo ambalo linafananishwa kwamba labda huenda alijitabiria kutokea kwa tukio hilo.

Tayari mmoja wa watoto wake amethibitisha kifo cha mtabiri huyo kutokea na kudai amefia hospitali akiwa anatibiwa, hivyo kuahidi taarifa zaidi zitatolewa hapo baadaye.
Soma habari zaidi/kamili ya kifo hiki hapo baadae; hppt://www.thehabari.com