Uasilia wa Jiji la Dar unavyotoweka taratibu

Kuibuka kwa maghorofa kila uchao! Huu ni moja ya mitaa ya katikati ya Jiji La Dar es Salaam na kinachoonekana juu ni baadhi ya maghorofa yanayojengwa baada ya kubomolewa majengo ya zamani.

Kuibuka kwa majengo mapya huku mtindo wa kuvunja yale ya asili kunaibadilisha Dar es Salaam na kila uchao kuonekana mpya. Changamoto iliyopo ni kufikiria na kutathimin je, kuna umuhimu wowote wa kulinda uhalisia wa jiji hili maarufu nchini Tanzania?

Majengo mapya yanayochipukia baada ya kubomolewa yale ya zamani jijini Dar es Salaam.