Serikali yaweka mpango kwa sekta binafsi kusaidia kukuza uchumi

Waziri wa Fedha na Uchumi MUSTAFA MKULO akiteta jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF ESTHER MKWIZU wakati wa semina iliyoandaliwa na TPSF ili kuhamasisha Watanzania kubuni miradi inayokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, TONIA KANDIERO akizungumza na washiriki wa Semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF ili kuhamasisha Watanzania kubuni miradi inayokopeshwa na benki hiyo.

Waziri wa Fedha na Uchumi MUSTAFA MKULO akisisitiza jambo kwa baadhi ya washiriki wa semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF ya kuhamasisha Watanzania kubuni miradi inayokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema imeweka mpango kabambe unaohusisha sekta ya umma na sekta binafsi kuweza kushirikiana ili kuweka vivutio vingi vitakavyowezesha nchi kukuza uchumi wake na wa mtu mmoja mmoja kupitia fursa mbalimbali za kiuwekezaji zilizopo.

Akizungumza kwenye semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kubuni miradi inayokopeshwa na benki hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo amesema sheria inatoa fursa kwa wadau kuitumia benki hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, BI. Esther Mkwizu amesema awali Watanzania walikuwa hawajui kama kuna utaratibu wa miradi ya watu binafsi kuweza kukopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika.