SHIBUDA AMWAGA CHECHE!!

Mbunge wa Maswa Mashariki, Mh. John Shibuda

Na Mwandishi Wetu
Mwanza
 
MBUNGE wa CHADEMA jimbo la Maswa Mashariki John Shibuda amesema CCM haikujivua gamba bali uzalendo baada ya kuuza nchi kwa mikataba mibovu na kuwaacha Watanzania wakiteseka kwa umasikini  na huduam mbovu za jamii..


Alidai endapo angechaguliwa kuwa Rais wa Tanzania mwajka jana  angehakikisha kuwa ndani ya kipindi cha miezi sita angemaliza uozo uliopo nchini ikiwa ni pamoja na kuwachulia hatua wtendaji wabovu waliosaini mikataba inayowaumiza wananchi kwa kuporwa rasilimali zao.

 
Mbunge huyo  wa Jimbo la Maswa Mashariki kupitia CHADEMA  alitoa kauli hiyo jana wakati akiwahutubia wananchi wa  kijiji cha Lamadi Jimbo la Busega kuwashukuru kwa kupigia kura chama hicho katika uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Alisema CCM kujivua gamba ni uprofesa wa uongo na katu chama hicho hakiwezi kuwaletea maisha bora  Watanzania, badala yake ni kuwaletea uchafu, dhuluma na maisha magumu kwani viongozi wake hawaaminiki kutokana na chama hicho kuwa na mashindano ya ulafi.

“CCM wamejivua gamba la uzalendo na kuuza nchi kwa mikataba mibovu na
kuwafukarisha wananchi, ina maprofesa wa kusema uongo,wabunge na madiwani wake wamebaki kuwa watu wa posho si wa kuwatetea ninyi.

 
Kumbukeni utamu wa kuku huanzia utotoni  leo wanasema wanajivua gamba” alisema Bw.Shibuda na kudai  ukweli uan tabia ya kuudhi masikio ya mtu dhulumati.

Aliwaeleza wananchi wa jimbo la Busega kuwa CCM na serikali yake imebaki na viongozi wala rushwa urithi ambao umerithiwa na Watendaji wa vijiji na Kata  kwa kuchangisha wananchi michango isiyo na tija.

Mbunge huyo aliwataka wananchi kuaondokana na fikra za nduho tabhu kwani CCM tayari imekiri kuwa chakavu ndiyo maana wamejivua gamba na kuifananisha  sawa na jiwe bovu lililokataliwa na waashi.Kwamba CCM  ni gulio la uongozi hawazingatii
haki za jamii na katiba ya nchi.

Bw.Shibunda alisema CCM kujivua gamba baada ya ubaini kuwa wao ni chakavu wamewapa mafisadi siku 90 lakini baadaye Katibu Mkuu, Wilson Mukama na Katibu Uenezi Nape Nauye wamepingana baada ya kula tumbaku ya rushwa kutoka kwa mafisadi, hivyo kuzidi kusambnaratisha chama chao.

“Utabiri wa Hayati Baba wa taifa,Mwalimu Nyerere umeanza kutimia, alisema
upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na Chadema kitakuwa chama kikubwa cha upinzani kutokana na sera zake nzuri,CCM sasa inakufa jiungeni na CHADEMA jeshi la wakovu kwa kuacha kura za mazoea kwa sababu CCM haina fadhila wala huruma na urithi wa watoto wenu” alisema .Shibuda

Kwamba CCM walipomfanyia fuko alijiondoa na kurudi nje ya kumi na nane na
kuwafunga  goli sawa na mchezaji wa Chelsea Drogba baada ya kumwonyesha kadi
nyekundu bila mpira na kusema katu moto wa chama chake kipya CCM hawataweza
kuuzima kwa chafya ya mpishi jikoni.

Alisema CCM ni sawa na agano la kale huku akiifananisha CHADEMA na agano jipya 
na kusema viongozi wa chama hicho cha zamani wanakula nchi yetu  kwa
kushirikiana na watalaamu wao na kuwafanya wananchi kuwa watumwa ndani ya nchi
ya  kiasi cha kupewa vyandarua va msaada.

Alieleza kwamba CCM na serikali yake  imefunga maendeleo ya wananchi na haina
mbinu ya kuondoa matatizo yao kwa viongozi wake wana mawazo mgando,na kudai kuwa
chama hicho ni jeneza la maziko ya matumaini na matarajio ya Watanzania,kutokana
na serikali yake kufuja rasilimali za nchi.

Bw Sibunda aliendellea kuhoji kuwa  ni kwa nini Baba wa taifa Mwalimu Nyerere
alitaifisha mali za mabwanyenye na leo ni miaka 50 CCM haijaweza kuwaletea
maisha bora,Watanzania na kuwafanya waendelee kwa sababu kinawadhulumu
rasilimali zao,hivyo akawataka waiondoe CCM madarakani kwa kuchagua chama chenye
matumaini ya wokovu.

“Chadema ni chaguo jipya na jeshi la wokovu, ni nuru ya ukombozi hivyo
muondokane na fikra za nduho tabhu,ufunguo wa maisha mazuri ni tabia
nzuri,tayari CCM imekiri kuwa ni chuma chakavu ndiyo sababu wamejivua gamba, ni
sawa na jiwe bovu lililokataliwa na waashi, kwa nini mnaling’ang’ania likataeni
likae katika nyumba zetu? Alihoji mbunge huyo wa Chadema.

“Wanaokula nchi na rasilimali zetu ni viongozi wa serikali na wataalamu wao,eti
wanasheria, uzalendo wao ni upi , ni uzandiki na dhuluma, serikali inasema
inawajibika kwenu kwa mujibu wa Katiba waongo, shughuli za uchumi hazuiendeshwi
kujilimbikizia mali.Ndiyo sababu waliponifania fujo nikasea utelezi wa mlenda
hamwuangushi mtu mzima na chafya ya mpishi haizimi moto wa jiko”

Bw. Shibuda alisema kwamba wabunge wa chama chake waliikataa rasimu ya katiba,
kwani mawaziri wa serikali ya CCM hawailindi Katiba hiyo ya nchi  waliyoapa
kuilinda ikiwa ni  wabunge wake, nao watekelezi matakwa ya katiba hiyo ambayo
inaelekeza kuwa kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali  na wananchi ndiyo mambo
yote, ili kukidhi misingi ya demokrasia

Alizidi kusisitiza kuwa alipojiondoa ndani ya CCM walifarakana na kumwita Ilogi
(mchawi) na sasa imebaki sawa na gunia tupu haiwezi kusimama, huku rasilimali za
Tanzania zikiliwa na wageni na kundi la wachache ndani  ya chama hicho na
kukifanya kiwe cha dhuluma kisimamia mateso yaliyopo, hivyo ukaidi huo hauwezi
kujenga nchi hii.

Mbunge huyo aliwataka wananchi kuchagua viongozi wenye uwezo wa kutumikia jamii
si kwa uwezo wa fedha zao kwa kuwa demokrasia ya CCM ni kuitikia amina
unapoibiwa ama dhulumiwa na kuambiwa vuta subira.

Awali Katibu CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Shilungushela Nyagaki alisema kuwa
matatizo ya watanzania yanatokana jinsi tulivyocagua wawakilishi wet na kuwataka
wananchi kubadilika kwa kuchaga mwakilishi bila kujali fedha alizo nazo. 

Katika mkuano huo CHAEMA ilivuna wanachama wapya 132 kutoka vyama mbalimbali
wakiwemo baadhi ya viongozi  32 wa CCM kutoka jimbo la Busega.Bw.Shibuda
ataendelea na ziara yake katika maeneo mbalimbali ya Kanda Ziwa baadaye mikoa
mingine baada ya kuopata mialiko 300.

mwisho